Friday, 4 March 2016

Chanzo Rasmi Cha Kifo Cha Mtoto wa Whitney Houston Bobbi Kristina Chafahamika...

Chanzo rasmi cha kifo cha Bobbi Kristina Brown kinakaribiana na kile cha mama yake, Whitney Houston – kuzama kwenye maji baada ya kutumia madawa ya kulevya Bobbi Kristina alikufa kutokana na kuzama kichwa chake kwenye maji baada ya kuwa ametumia mchanganyiko wa madawa.

Umebaini vitu alivyokuwa ametumia ni bangi, pombe, madawa yenye uhusiano na cocaine, benzoylecgonine, benzodiazepines na morphine. Ripoti imedai kuwa alifariki kutokana na kupata The pneumonia na encephalopathy – kwamba mapafu yake yalijaa maji na ubongo wake ulijeruhiwa.

Kifo cha Whitney kilitokana na kuzama kwenye bafu katika hoteli ya Beverly Hilton, kulikochangiwa na cocaine na ugonjwa moyo. Bobbi Kristina alifariki July 26 baada ya kukaa miezi kadhaa mahututi. Alikuwa na miaka 22.

No comments:

Post a Comment