LEO
Feb 17 2016, Mke wa Rais John Pombe Magufuli Janeth Magufuli amewasili
katika shule ya msingi Mbuyuni, Dar kwa ajili ya kuagana na
walimu wenzake pamoja na wanafunzi aliokuwa akiwafundisha
Shule ya Msingi Mbuyuni ni shule
ambayo Mama Magufuli alisoma kuanzia darasa la kwanza na baadaye mwaka
1995 kurudi tena kufundisha hapohapo kwa miaka 17 hadi mumewe Rais Magufuli alipochaguliwa kuwa Rais wa Tanzania.
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akipokea zawadi ya saa toka kwa mwalimu
Mkuu wa shule ya Msingi ya Mbuyuni, Mwalimu Dorothy Mwalecela ,
Oysterbay, jijini Dar es salaam wakati wa sherehe fupi ya kuwaaga rasmi
walimu wenzake na wanafunzi wa shule hiyo
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akisikiliza risala toka kwa mwanafunzi wa
shule ya Msingi ya Mbuyuni Oysterbay, jijini Dar es salaam wakati wa
sherehe fupi ya kuwaaga rasmi walimu wenzake na wanafunzi wa shule hiyo
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akipokea zawadi toka kwa Afisa Elimu wa
Wilaya ya Kinondoni katika Shule ya msingi ya Mbuyuni Oysterbay, jijini
Dar es salaam wakati wa sherehe fupi ya kuwaaga rasmi walimu wenzake na
wanafunzi wa shule hiyo
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akisikiliza maelezo ya utangulizi ya
mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi ya Mbuyuni, Mwalimu Dorothy Mwalecela ,
Oysterbay, jijini Dar es salaam wakati wa sherehe fupi ya kuwaaga rasmi
walimu wenzake na wanafunzi wa shule hiyo




No comments:
Post a Comment