Tuesday, 23 February 2016

Video: Msikilize Jerry Muro Akiwajibu Wanaosema Yanga Kabebwa na Refa Katika Mechi Dhidi ya Simba



Jumamosi ya February 20 ulipigwa mchezo wenye upinzani na historia kubwa katika nchi hii, hiyo ndio siku ambayo ulipigwa mchezo wa Simba na Yanga, huu ulikuwa mchezo wa marudiano wa Ligi Kuu Tanzania bara, mchezo ambao ulimalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Simba. Lakini kuna baadhi ya mashabiki wa Simba wanasema refa aliipendelea Yanga na kumuonesha kadi nyekundu Abdi Banda.

Afisa habari wa Yanga Jerry Muro ana majibu haya kwa wale wanaosema Yanga ilipendelewa >>> “Baadhi ya mashabiki tumewasikia kwenye vyombo vya habari wakilalamika Yanga ilipendelewa, lakini niwaambie kocha wao ambae ni mtaalam Jackson Mayanja amehojiwa leo lakini hakusema refa alipendelea na kueleza kuwa kafungwa kwa sababu hesabu zake zilikataa, sasa wao na kocha nani mtaalam?”

Hii ndio video unaweza kumuangalia Jerry Muro akieleza kwa kirefu

No comments:

Post a Comment