1. Utangulizi
Mnamo mwezi Februari mwaka 2015, serikali ya Tanzania ilizindua sera mpya ya Elimu na Mafunzo.
Sera hii imepanua wigo wa elimu ya msingi kwa kuiunganisha na elimu ya sekondari (hii ilikuwa ikitolewa bure na kwa lazima tangu mwaka 2001 baada ya kuanzishwa kwa Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi {MMEM}).
Sera hii imepanua wigo wa elimu ya msingi kwa kuiunganisha na elimu ya sekondari (hii ilikuwa ikitolewa bure na kwa lazima tangu mwaka 2001 baada ya kuanzishwa kwa Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi {MMEM}).
Tangu
kuchaguliwa kwa Rais John Pombe Magufuli mwezi Octoba mwaka 2015,
utekelezaji kikamilifu wa sera hii imekuwa moja ya ahadi kuu za serikali
yake.
Rais
Magufuli aliwahakikishia wazazi wenye watoto wanaosoma katika shule za
msingi na sekondari katika hotuba yake ya ufunguzi wa bunge la kumi na
moja kuwa hawatapaswa kutoa michango yoyote kuanzia mwezi Januari mwaka
2016.
Rais
Magufuli pia alibainisha kuwa fedha zote zitakuwa zikipelekwa moja kwa
moja shuleni, na kuongeza kuwa “Nina uhakika fedha hizo zitatumika
vizuri, ole wao watakao zitumia vibaya.”
Japokuwa
dhamira hii ya kutoa elimu bure mpaka kiwango cha sekondari (kidato cha
nne) kwa kila mtoto wa Kitanzania ni hatua kubwa katika historia ya
nchi, lakini upatikanaji fursa za elimu siyo changamoto pekee
inayoukabili mfumo wa elimu nchini Tanzania. Juhudi zote zitakuwa hazina
maana kwa wananchi na taifa kwa ujumla iwapo watoto wanaenda shule
lakini hawajifunzi.
Hivyo
basi ubora wa elimu inayotolewa ni suala muhimu pia. Ripoti ya Uwezo ya
mwaka 2014 inaonesha kuwa asilimia 19 pekee ya wanafunzi wa darasa la 3
ndiyo walioweza kusoma hadithi ya Kiingereza ya kiwango cha darasa la
pili 4 .
Tukiangalia
ufaulu wa darasa la 7 mwaka 2015, takribani asilimia 68 ya wanafunzi
waliofanya mitihani walifaulu 5 . Japokuwa hii ni ongezeko la ufaulu kwa
karibu asilimia 11, bado ni idadi kubwa ya wanafunzi wasiofaulu
ipasavyo.
Kutokana
na umuhimu wa elimu katika maendeleo, na ukizingatia mabadiliko katika
sekta ya elimu yanayoendelea nchini hivi sasa, ni vyema kufahamu
mitazamo ya wananchi kuhusu mfumo wa elimu ya umma.
Wananchi
wana mtazamo gani juu ya hali ya elimu iliyopo hivi sasa? Wana maoni
gani juu ya walimu wa shule za umma na ubora wa elimu wanayopatiwa
watoto wao? Je wana matarajio yapi kuwa elimu ya bure itaboresha elimu?
Je
wazazi wamekuwa wakichangia fedha kiasi gani huko mashuleni, na nini
athari za kupigwa marufuku kwa michango yote ya wazazi katika elimu? Na
je fedha hizo zimetumikaje?
Muhtasari
huu umebeba maoni na uzoefu wa wananchi juu ya utolewaji wa elimu ya
msingi ya umma. Tunatumaini matokeo haya yatakuwa mwanzo mzuri wa kupima
mafanikio ya utekelezaji wa sera hii mpya kwa siku za usoni.
Takwimu
kutoka muhtasari huu zimekusanywa na Twaweza kupitia mpango wake wa
Sauti za Wananchi. Sauti za Wananchi ni utafiti unaofanywa kwa njia ya
simu za mkononi, wenye uwakilishi wa kitaifa. Utafiti huu unawakilisha
Tanzania Bara.
Mambo muhimu kuhusu matokeo haya:
• Asilimia 76 ya wananchi wanaamini kuwa utoaji wa elimu bure utaboresha elimu.
• Asilimia 89 ya wazazi wanasema wanatoa michango ya fedha kugharamia elimu ya watoto wao waliopo shule za umma.
• Asilimia 66 ya michango ya wazazi hulipia ulinzi, asilimia 57 majaribio na asilimia 34 madawati.
• Karibu nusu ya wananchi wanaamini michango inayokusanywa shuleni haitumiki kwenye malengo husika.
• Wananchi 8 kati ya 10 wanaamini kuwa walimu hawapendi taaluma yao.
•
Nusu ya wananchi wote wanaona kuwa ubora wa elimu ya msingi umezorota
ama kubaki pale pale wakati nusu nyingine wanaona kuwa imeboreshwa. Hii
ni ndani ya miaka 10 iliyopita.
2. Mambo sita kuhusu elimu nchini Tanzania
Jambo la 1: Wananchi wana matumaini na ahadi ya elimu bure
Asilimia
97 ya wananchi wanafahamu kuhusu ahadi ya Rais Magufuli ya kutoa elimu
bure ya sekondari (kidato nne) kuanzia Januari 2016, kama ilivyoainishwa
kwenye sera mpya na ilani ya chama tawala. Vilevile, asilimia 88 wana
imani kuwa ahadi hii itatekelezwa kama ilivyopangwa.
Asilimia
76 ya wananchi wanaamini kuwa utolewaji wa elimu bure utaongeza ubora
wa elimu kwa kuboresha mazingira ya kufundishia (asilimia 55).
Pamoja
na imani hiyo, asilimia 15 ya wananchi walisema elimu ya bure
haitaboresha elimu, kwa kuwa kuongezeka kwa uandikishwaji wa wanafunzi
kutatumia rasilimali (fedha) nyingi 8.
Asilimia
49 walisema wanafunzi hawatafanya vizuri kutokana na kukatazwa kwa
masomo ya ziada ambayo walimu waliyatumia kuwasaidia wanafunzi
wasiofanya vizuri huku wakijipatia kipato cha ziada. Pamoja na hayo
asilimia 22 wana hofu na upatikanaji wa vifaa vya kutosha vya
kufundishia 9 .
Jambo la 2: Asilimia 89 ya wazazi huchangia elimu ya umma
Michango
imekuwa ni sehemu ya mfumo wa elimu baada ya upanuzi wa Elimu ya Msingi
kwa Wote. Asilimia 89 ya wazazi waliohojiwa walikiri kuchangia fedha
kwenye shule za umma.
Wazazi
walipoulizwa kuhusu kiwango cha fedha walichochangia, asilimia 80
walisema wamechangia TZS 50,000 ama pungufu kwa mwaka, huku asilimia 8
wakichangia zaidi ya TZS 100,000 .
Michango
inayotolewa kwenye shule za umma hutumika kugharamia ulinzi (asilimia
66), majaribio (asilimia 57) na madawati (asilimia 34). Kiwango kidogo
hutumika kwenye mahafali (asilimia 4) na safari za kishule (asilimia 4).
Utaratibu
wa ugawaji wa fedha za ruzuku ni: asilimia 40 vitabu na nyenzo nyingine
za kusomea; asilimia 20 kwa ajili ya vifaa vya kuandikia (kalamu,
madaftari, penseli n.k.); asilimia 10 kwa shughuli za kiutawala na
asilimia 10 kwa ajili ya makaratasi ya mitihani na uchapishaji. Hivyo
basi, maamuzi ya kuwa ruzuku itumike vipi yanakuwa changamoto kwa upande
wa shule zenyewe, na hata hivyo, inaonekana wazi kuwa michango hulipia
vitu vingi zaidi kuliko ruzuku.
Jambo la 3: Asilimia 49 ya wazazi wanaamini michango ya wazazi haitumiki ipasavyo
Japokuwa
wazazi wengi wamekuwa wakitoa michango ya ziada, asilimia 49 ya wazazi
wanaamini kuwa fedha hizo hazitumiki ipasavyo. Wazazi wa mjini wana
mashaka zaidi ambapo asilimia 57 wanasema hivyo ukilinganisha na
asilimia 44 ya wazazi wa vijijini.
Vilevile
asilimia 58 ya wananchi wanaamini kuwa michango hii haijaidhinishwa na
serikali. Asilimia 89 wanaamini kuwa walimu wa shule za umma huchangisha
fedha hizo kama chanzo cha kujipatia kipato cha ziada 11 .
Jambo la 4: Wananchi wanahusisha mafanikio ya ujifunzaji na juhudi za mwalimu
Wananchi
walipoulizwa kuwa ni nini ambacho wanadhani kinachangia matokeo ya
darasa la saba kwenye jamii yao (kuwa mazuri ama mabaya), nusu yao
walihusisha matokeo na juhudi za mwalimu 12 . Asilimia 7 pekee ndio
waliotaja changamoto zinazohusiana na wazazi au wanafunzi wenyewe 13 .
Cha
kushangaza ni kwamba mwananchi 1 kati ya 3 hajui nini kinachangia
matokeo ya kujifunza pindi watoto wanapohitimu elimu ya msingi.
Jambo la 5: Wananchi wanaamini kuwa walimu wanaona fahari juu ya taaluma yao lakini hawapendi kazi yao
Asilimia
93 ya wananchi wanaamini kuwa ualimu ni taaluma ambayo ndiyo msingi wa
taifa. Japokuwa asilimia 79 ya wananchi wanaamini kuwa walimu wanaona
fahari ya kile wanachokifanya, asilimia 80 wanaona kuwa walimu hawapendi
kazi zao na hufanya tu kwa ajili ya kujipatia kipato. Je ni kwanini
walimu wanaona fahari ya taaluma yao lakini hawapendi kazi yao?
Kwa
mujibu wa baadhi ya wananchi, ni kutokana na mishahara pamoja na
mazingira ya kufanyia kazi. Kwa ujumla asilimia 42 ya wananchi wanaamini
kuwa walimu hawalipwi vizuri, na asilimia 34 wanaamini mazingira ya
kazi ya walimu hayawapi motisha wa kufundisha.
Haya
ni maoni ya wananchi wachache (wananchi wengi wanatoa kauli
zinazokinzana), lakini yanaweza kutoa mwanga kwanini wananchi wanadhani
walimu hawapendi kazi yao.
Wananchi
walipoulizwa kuhusu vitu ambavyo vinaweza kuwaongezea walimu motisha
ili kutoa elimu bora kwa wanafunzi, asilimia 56 walisema nyongeza ya
mishahara na asilimia 19 walitaja uboreshaji wa mazingira ya kazi.
Jambo la 6: Maoni ya wananchi yanatofautiana juu ya ubora wa elimu ya msingi.
Wananchi
walipoulizwa kuhusu ubora wa elimu, nusu yao waliamini kuwa ubora wa
elimu ya msingi umezorota ama kubaki vilevile kwa kipindi cha muongo
mmoja uliopita, huku nusu nyingine wakisema elimu ya msingi imeboreshwa.
Wananchi
walio wengi wanaamini njia kuu ya kuboresha elimu ya msingi ni kwa
kuweka mkazo kwa walimu. Ili kuboresha elimu wananchi wametoa ushauri
ufuatao kwa serikali: kufuatilia utendaji wa walimu (asilimia 40),
kuongeza mishahara ya walimu (asilimia 19), pamoja na kuongeza idadi ya
walimu (asilimia 10). Asilimia 7 pekee ndiyo waliotaja ushirikiano kati
ya
mwalimu na mzazi kama njia ya kuwawezesha watoto kujifunza.
3. Hitimisho
Serikali
mpya imejikita kwenye utoaji wa elimu bure kwa shule za msingi na
sekondari na wananchi wamekuwa na imani kubwa juu ya suala hilo.
Wananchi wanaamini kuwa utoaji wa elimu bure utatekelezwa katika muda
ulianishwa, na ubora wa elimu utaongezeka.
Wasiwasi
wa wananchi unaonekana kwenye uwajibikaji wa walimu katika kufikia
kiwango cha juu cha elimu. Walipoulizwa kuhusu namna ya kuboresha elimu
ya msingi, wananchi walitilia mkazo kwenye mishahara ya walimu,
kuongezeka kwa idadi ya walimu mashuleni na zaidi ya yote uwajibikaji
wa walimu.
Siyo
wananchi pekee wanaosisitiza uwajibikaji wa walimu. Kwa mujibu wa
Davidson, ukosefu wa motisha kwa walimu ni moja ya sababu kuu
inayoathiri ubora wa elimu nchini Tanzania 16 .
Utafiti usio rasmi uliofanywa na Twaweza kwa walimu 272 unaonesha kuwa asilimia 96 ya walimu hao hawaridhishwi na kazi zao.
Pia,
mwalimu 1 kati ya walimu watatu alisema asingechagua tena kazi ya
ualimu, huku wakitaja mazingira magumu ya kazi (asilimia 34) na
mishahara midogo (asilimia 26) kama sababu kuu. Hii inadhihirisha kuwa
walimu na wananchi kwa ujumla wana mitazamo inayofanana.
Kwa
kuwa uongozi mpya umeweka mkazo suala la elimu, ni vizuri pia ukaanza
kutatua matatizo ya walimu na kuboresha mazingira ya ufundishaji
Tanzania ili kwenda sambamba na kasi ya utoaji wa elimu.
Wakati utekelezaji wa sera mpya ya Elimu ukiendelea, ni vyema kufuatilia mabadiliko yaliyofanyika na mafanikio yaliyopatikana.
Kumekuwa
na kusitasita kuhusu dhana hii ya ‘elimu bure’ ambapo viongozi wa shule
wana mashaka na jinsi ambavyo TZS 10,000 kwa kila mwanafunzi mmoja kwa
mwaka inaweza kutosha. Mfano mmoja ni kuhusu suala la ulinzi.
Kama
ilivyoelezwa hapo juu, asilimia kubwa ya michango ya wazazi kwa mwaka
2015 imekuwa ikitumika kwenye ulinzi (asilimia 66); wakati ruzuku
inayotumwa shuleni haihusishi suala la ulinzi.
Iwapo
fedha zote zilizotengwa zitapelekwa shuleni na kuwafikia wahusika kwa
kiwango kilichopangwa, je kiwango hicho kitatosha kuhakikisha watoto
wanajifunza?
Suala
jingine la msingi ni kuhusu utunzwaji wa rasilimali. Ruzuku hapo awali
zilikuwa zinapelekwa moja kwa moja shuleni mpaka mwaka kufikia mwaka
2002 zilipoanza kupelekwa kupitia kwa mamlaka zaHalmashauri za Wilaya na
Miji.
Kwa
sasa mfumo umebadilika ambapo ruzuku zinapelekwa moja kwa moja shuleni.
Tunaamini uamuzi wa kupeleka ruzuku moja kwa moja mashuleniumechangiwa
na na kutokuwepo kwa ufanisi katika mfumo uliopita.
Kwa mfano, kati ya 2010 na 2013, kwa wastani ni TZS 2,202 pekee ndizo zilizofika shuleni kwa kila mwanafunzi.
Sera
mpya ya kupeleka pesa za ruzuku moja kwa moja mashuleni unaibua maswali
kadhaa. Tutahakikisha vipi upelekaji wa pesa moja kwa moja kwenye shule
utatupa matokeo tofauti?
Je
shule zina uwezo wa kusimamia rasilimali hizo vizuri; kuzuia ubadhirifu
na upotevu na kuhakikisha zinaelekezwa kwenye matumizi ya vitu muhimu
zaidi? Kuna mfumo gani uliopo kwenye ngazi ya shule, hususani katika
kuhakiki maamuzi ya matumizi?
Ili
kuhakikisha tunapata thamani halisi ya matumizi katika elimu, utoaji na
matumizi ya fedha vinapaswa kuhakikiwa katika ngazi ya shule.
Kwa
kumalizia, na la muhimu zaidi, utawala mpya umeonekana kuwa kimya
kwenye suala la kuboresha matokeo ya ujifunzaji. Ongezeko la shule za
msingi kwa mamilioni ya watoto wa kitanzania ni mafanikio makubwa.
Hata
hivyo, baada ya miaka kumi ya sera hii, tunatilia shaka anguko la
uandikishaji huo wa maelfu ya watoto pasipo kutoa fedha za kutosha, wala
kutilia mkazo suala la ubora. Je kutakuwa na walimu wa kutosha kwa
wanafunzi hawa? Tutahakiki vipi kama wanajifunza?
Kwa
kipindi cha miaka kumi iliyopita tumeshuhudia ongezeko kubwa la shule
za sekondari pamoja na wanafunzi huku ikiambatana na ongezeko kubwa la
idadi ya wanafunzi wanaofanya vibaya kwenye mitihani yao ya kidato cha
nne.
Je uongozi huu umejipanga kufanya nini cha tofauti kuhakikisha kuwa Tanzania haiendelei kutengeneza wahitimu mbumbumbu?
Tutahakikisha
vipi mfumo wa elimu unawapa watanzania fursa ya kuishi maisha mazuri na
kuchochea maendeleo ya nchi? Pamoja na nia njema na maelezo mazuri ya
Rais yanayotilia mkazo kwenye elimu na kutoa matumaini mapya, ni muhimu
kuzingatia kuwa ufanisi katika sekta hii muhimu utafikiwa kwa kutumia
ushirikiano na wadau wote.
Aidha,
panahitaji marekebisho mapana zaidi katika mfumo wa elimu ili kufikia
malengo ya elimu bure na bora, na sio bora elimu bure!
No comments:
Post a Comment